Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa mwezi Machi, wasanii kutoka Tanzania wameendelea kukosha na kuburudisha mashabiki zao kwa ngoma mpya na kali. Kutoka kwa wasanii kama Kontawa, Gigy Money, Barnaba Classic na wasanii wengine wengi hizi hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii :

Dunga Mawe - Kontawa

Kontawa ana kipaji kikubwa sana,hasa linapokuja suala la kuandika mashahiri na ngoma yake hii mpya ya kuitwa Dunga Mawe imethibitisha hilo.  Kwenye Dunga Mawe, Kontawa anamuelezea rafiki yake wa utotoni aliyeitwa Dunga Mawe na kwenye ngoma hii utapata burudani, mafunzo na mambo mengi kuhusu maisha

Nampenda - Barnaba Classic

Barnaba amerudi tena na “Nampenda”. Humo ndani ameongelea kuhusu mapenzi lakini kubwa zaidi amerusha mawe na kuwatolea uvivu watu wanaomsema vibaya na kufuatilia maisha yake.

 

Ogopa - Gigy Money

Kama unapenda kusheherekea maisha na kufurahi basi Gigy Money amekuletea hii ya kuitwa Ogopa. Humu ndani Gigy ametembea kwenye beat safi la Amapiano ambalo bila shaka litasikika sana kwenye kumbi mbalimbali za starehe Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=GicZHA4V0EQ

Ramadan - Yammi

Kwenye ngoma yake hii mpya Yammi anasheherekea mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kuwagasa waumini  wote wafunge na kufanya matendo mema katika mwezi huu.

https://www.youtube.com/watch?v=biP-b-hIYgU

Hata Sijui - Motra The Future Ft Kontawa

Kwenye ngoma hii ya rap utapenda namna ambavyo Motra The Future ameongelea mambo mengi ndani ya dakika tatu. Humu ndani Motra amezungumzia kuhusu BASATA, kiki kwenye muziki na mambo mengine yanayoendelea kwa sasa.

https://www.youtube.com/watch?v=N1vk_1TVrM8

Leave your comment