Country Wizzy Akosha Mashabiki na Ngoma Mpya 'No (Interlude)'

Download FREE Mp3 Music by Country Wizzy on Mdundo.com

Msanii kunako kiwanda cha Hip Hop nchini Tanzania, Country Wizzy, hivi karibuni amewakosha mashabiki zake baada ya kuachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa No (Interlude) 

Country Wizzy ambaye miaka ya nyuma alikuwa kwenye lebo ya Konde Gang ameachia ngoma hii ya No (Interlude) ikiwa ni takriban miezi mitatu tangu aachie “One Call Away” ngoma ambayo pia ilipokelewa vyema na mashabiki. 

Kwenye “No Interlude” Country Wizzy anatoa ushauri na maneno mazito kwa watu wasiomtakia mema ambapo kupitia mistari yake Country Wizzy anaoneshwa kukerwa na watu wanaofuatilia maisha yake. Ukiweka kando mashahiri ya ngoma kuwa ya kipekee lakini pia mdundo wake bila shaka utapendwa na mashabiki wengi.

Ngoma hii imetayarishwa na producer Wambaga kutoka Tanzania ambaye pia amehusika kutayarisha ngoma ya Shy ya kwake Cukie Daddie akiwa amemshirikisha Sai Kenya. 

 

Leave your comment