Nyimbo Mpya Kutoka Tanzania Wiki Hii

Join our WhatsApp channel to Receive latest news, New MP3s & DJ Mixes

Kuanzia kwenye Bongo Fleva mpaka kwenye muziki wa Hip Hop, itoshe kusema kwamba ndani ya wiki hii wasanii kutoka Tanzania wameweza kuachia ngoma kali zenye lengo la kukosha na kuburudisha mashabiki wa muziki Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Kutoka kwa wasanii kama Ali Kiba, Nay Wa Mitego, Maarifa  na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii : 

La la la - Ali Kiba Ft Vanillah, K2ga, Abdu Kiba & Tommy Flavour 

Mdundo mkali kutoka kwa Yogo Beats umechagiza ngoma hii ya La La La kuwa kali sana. Ndani ya wimbo huu, Kings Music wanazungumzia kuhusu mapenzi na namna ambavyo wanapata raha na furaha kutokana na kupendwa na wapenzi wao. 

Kudadadeki - Nay Wa Mitego 

Wengi wanamfahamu Nay Wa Mitego kama msema ukweli na kwenye ngoma yake mpya ya kuitwa Kudadadeki, rapa huyo ameendeleza utamaduni wake huo wa kuzungumzia yanayotokea kwenye jamii. 

Kudadadeki ni ngoma ambayo Nay anazungumzia kuhusu maisha ya mtaani kwa ujumla wake. 

Freestyle - Nyandu Tozzy Ft Wiz Tyson 

Baada ya ukimya wa takriban mwaka mmoja, Nyandu Tozzy ameamua kuungana na Wiz Tyson kuileta Freestyle. Kwenye Freestyle utapenda michano mikali ya Nyandu Tozzy pamoja na mashahiri mazuri yaliyomo kwenye ngoma hii 

Anameremeta - Lulu Diva, Khadija Kopa, Mwasiti, Mimi Mars,Phina 

Anameremeta umefanyika pale Tongwe Records chini ya producer Bin Laden. Kwenye kibao hiki Lulu Diva anaungana na wasanii wenzake kumsifia na kumpa pongezi Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake kwenye jamii. 

 

Nikilala - Mocco Genius 

Kwenye ngoma yake hii mpya, Mocco Genius anahadithia mashabiki zake namna ambavyo anateseka kutokana na kuachwa na mpenzi wake aliyempenda sana. Humu ndani utapenda sauti nzuri ya Mocco Genius pamoja na ujumbe wa Mocco Genius kwa ujumla. 

Leave your comment