Kayumba Kuachia Albamu Mpya “Fine Tape”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Kayumba hivi karibuni ametangaza kuachia album yake inayokwenda kwa jina la Fine Tape.

Kayumba ambaye alianza kupata umaarufu baada ya kushiriki kwenye shindano la Bongo Star Search ametangaza kuachia albamu hiyo hivi karibuni na hivyo kupelekea mashabiki kusubiri kwa hamu mradi huo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kayumba alidokeza kuwa albamu yaka hiyo mpya itaitwa Fine Tape na itaachiwa leo Machi 2, 2023 na albamu hiyo inatarajiwa kuwa albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki.

Aidha “Fine Tape” itasindikizwa na uzinduzi mkubwa wa aina yake ambapo katika harakati za kuitangaza albamu hiyo, Kayumba amekuwa akifanya akidokeza kuhusu albamu hiyo kwa kuwasikilizisha ngoma zilizomo kwenye albamu hiyo wasanii tofauti ikiwemo Kusah, Whozu na wengineo wengi. 

Leave your comment