Aslay Adokeza Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama ulikuwa unasubiri ujio mpya wa msanii Aslay basi habari njema ni kwamba msanii huyo amedokeza iwamba muda si mrefu ataachia ngoma mpya.

Mara ya mwisho kwa Aslay kuachia ngoma ilikuwa ni Januari mwaka huu ambapo aliachia ngoma yake ya Inauma ambayo ilipokelewa kwa mikono miwili na mashabiki kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Aslay alidokeza kuhusu ujio wake mpya kwa kuandika

“Kuna zawadi nyingine inakuja wadau wangu mnivumilie tu kipindi hiki kitamu”

Ikumbukwe kuwa tangu aingie Rockstar Africa, Aslay tayari ameshaachia ngoma tatu ambazo ni Follow Me akiwa na Harmonize, Mozzah pamoja na Inauma

Leave your comment