Mkubwa Fella Akanusha Mavokali Kusainiwa Wcb Wasafi

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wakati mashabiki wakiendelea kushuku ni msanii yupi ambaye hivi karibuni amesainiwa kwenye lebo ya WCB, moja ya viongozi wa lebo hiyo, Mkubwa Fella amejitokeza hivi karibuni na kukanusha tetesi za kwamba Mavokali ndiye msanii mpya wa lebo hiyo.

Mkubwa Fella ambaye alikuwa ni meneja wa kundi la Ya Moto Band amejitokeza hivi karibuni na kusema kuwa Mavokali ambaye alidhaniwa na wengi kuwa amesainiwa WCB WASAFI sio msanii mpya wa lebo hiyo ambayo ni moja ya lebo kubwa sana Afrika

Ikumbukwe kuwa Februari 2 2023,  Diamond Platnumz alidokeza kuwa amesaini msanii mpya WCB baada ya kuchapisha sehemu ya mkataba wa msanii huyo kwenye Instastory yake.

Saa chache baadaye Mavokali nae alifuta post zake zote za Instagram na kupitia Instastory yake aliandika “Deal Done” kitu kilichofanya mashabiki kudhani kwamba Mavokali ndiye msanii mpya wa WCB Wasafi.

Hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na Dizzim Online, Fella alikanusha taarifa hizo kwa kusema

“Kwanza sio yeye alafu msanii anatoka Temeke ila simtaji itakapofika time mwenyewe atamtaja Naseeb”

Ikumbukwe kuwa Zuchu ndio msanii wa mwisho kutambulishwa kwenye lebo ya WCB Wasafi ambapo alitambulishwa takriban miaka mitatu iliyopita na tangu hapo WCB Wasafi hawajatangaza tena msanii mpya.

 

Leave your comment