Harmonize Adokeza Ngoma Na Bien Wa Sauti Sol

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama wewe ni stability wa Muziki mzuri basi bila shaka utafurahishwa na taarifa hii kutoka kwa Harmonize ambaye hivi karibuni amedokeza kuwa yuko mbioni kuachia ngoma na meaning Bien kutokea huko nchini Kenya

Harmonize ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Single Again ametoa taarifa hiyo hivi karibuni ikiwa ni siku change tangu ngoma ya Nobody  ambayo Darassa pia amemshirikisha Bien iingie sokoni

Kupitia ukurasa wake wa Instagram kipindi akiwa Live, Harmonize amedokeza kuhusu ujio wa ngoma hiyo na Bien kwa kuandika kuwa ngoma hiyo itaenda kuandika historia kwenye muziki.

“The Rest Will Be History this with BAD MAN take it from me and save the Date Inshaallah”  aliandika Harmonize kwenye ukurasa wake.

Ikumbukwe kuwa kutoka nchini Kenya, Harmonize hivi karibuni alishirikishwa kwenye ngoma ya Kwame na Khaligraph Jones, ngoma ambayo kufikia sasa imefikisha views zaidi ya Milioni 1.5 kwenye mtandao wa Youtube

Leave your comment