Yammi Arudi Kivingine Kwenye Video Yake Mpya Ya Tunapendezana

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Yammi anaendelea kuwaburudisha mashabiki zake bila kuchoka na juhudi zake zimeonekana tena hivi karibuni baada ya kuachia video ya Tunapendezena ambayo mashabiki wa muziki walikuwa wanaisubiri kwa hamu sana.

Muda mfupi uliopita Yammi ambaye yuko chini ya lebo ya The African Princess aliachia video ya Tunapendezana. Tunapendezana ni ngoma namba 2 kwenye EP yake ya kuitwa "Three Hearts" ambayo ilitoka mwezi Januari mwaka huu.

Video ya Tunapendezana imepambwa na stori nzuri ambapo Yammi wakati video inaanza anaonekana akiwa anafundwa na kungwi wa masuala ya ndoa na kutoka hapo katika mandhari tofauti tofauti, Yammi anaonekana akiwa anakula raha na mpenzi wake.

Video ya Tunapendezana imefanyika jijini Dar Es Salaam, Tanzania ikiwa imetayarishwa na Director Kenny. Ikumbukwe kuwa Director amehusika katika kutayarisha video za wasanii ikiwemo Sukari ya Zuchu, Jeje Ya Diamond Platnumz na Leave Me Alone ya Harmonize.

https://www.youtube.com/watch?v=ipj-j6GQomw

Leave your comment