Lyrics: Stamina Shorwebwenzi Ft. Bushoke - Machozi

[Image Source: Instagram]

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Oy niaje mwamba samahani nakusumbua

Naomba usikatae simu taratibu utanijua

Nampigia mke wangu naona hapokei simu

Ila najua umelala nae sorry na kukata stimu

Na unanijua na unajua si ni wazazi

Naumia kuona Wanangu wanalala na dada wa kazi

Na usiulize namba yako nimeitoa wapi

Naomba uskize mi ni mumewe wa ndoa na chati

Kwanza nikupe pongezi we mjasiri mi kulala na mke wa mtu siwezi

Unapata nguvu ipi kuipa hayo mamlaka a halo mume wake yu hai hajafa haja pa talaka

 

Alafu naskia na sound umechoka sana ndio mshamaliza round ya kwanza au sio mwana

Wakati mi nalala mito we unaenjoy unamkunja kama kiko

 

Vipi mtamu eeh kanona eeh

Nagharamika bro sijui kama unanisoma aisee

Najua unampenda sababu unamhudumia ukitaka nikuachie bro uone jinsi nnavyoumia

 

Kama kidume cha mbegu kesho nikuletee watoto uwalee

Na Mke wangu unipunguzie msoto inaniuma

Nimemhudumia nimempa thamani zamani nakuhakikishia ungemwons haungemtamani

 

Kama anasema ndoa imekuwa daah changamoto

Au anasema tumeachana anabaki tunalea watoto

Sorry salio inakata anaweka vocha nakupigia ili unipe simu niongee naye huyo mshenzi wa tabia

 

Kama binadamu nina moyo sio chumba naumia

Machozi yanitoka nashindwa vumilia

Natamani niondoke hata kwenye hii dunia

Maana heshima yangu we umeshindwa nitunzia

 

Unaniumiza moyo eeeh

Akili yangu haisomi eeeh

Umenishusha thamani eeeh

Nadharauliwa mtaani eeeh

 

Pole sana kwa uchovu pole kwa kazi nzito ya kubeba pombe ya ndovu

Najua ulipanga unidanganye boya lako kuwa party illisha late ukalala kwa shosti ako

Kukuita malaya sitoweza umeni alia watoto ila heshima unaipoteza

 

Japo mambo Unayo fanya kiasherati we sio smart

Umesahau una familia au na watoto huwataki

Okay tuseme sikuridhishi kitandani anayetoa kodi ya meza hapa nyumbani ni nani?

 

Unadhani watoto watakuwa tu sex yetu

Au nikikosa hela utalishwa na bwana Yesu

 

Zile make up kusuka wanna saluni

Ungezipata wapi nisingekaza kisa uni

Hata kama sio handsome nilitimiza majukumu

Sasa huyu atakuwa nini zaidi ya Kukulisha ndumu

 

Wazazi waliposema kuwa tukapime DNA

Nilisema wamezeeka hawa wazazi TZA

Sahivi naelewa kila nikiwacheki watoto sura yangu inakuja inaondoka changamoto

 

Ukirudi nyumbani chukua kilicho chako

Tena ikibidi nenda na watoto wako

Nauonea huruma huo mfuko wako wa uzazi

Ungekuwa mfuko wa kawaida ningeshaubebea viazi

 

Kama binadamu nina moyo sio chumba naumia

Machozi yanitoka nashindwa vumilia

Natamani niondoke hata kwenye hii dunia

Maana heshima yangu we umeshindwa nitunzia

 

Unaniumiza moyo eeeh

Akili yangu haisomi eeeh

Umenishusha thamani eeeh

Nadharauliwa mtaani eeeh

https://www.youtube.com/watch?v=djABvQoYiPQ

Leave your comment