Rapa Mwanafa Ateuliwa Kuwa Naibu Waziri Wa Sanaa, Utamaduni Na Michezo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mabadiliko yanaendelea kufanyika katika kiwanda cha burudani nchini Tanzania na hii ni baada ya rapa maarufu na Mbunge wa Muheza Mwana FA hivi karibuni kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Wa Sanaa, Utamaduni Na Michezo.

Uteuzi huo imefanyika siku ya Jumapili ya tarehe 26 Februari ambapo Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma ameteuliwa kwenye nafasi hiyo na Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Katika nafasi yake hiyo mpya ya Naibu Waziri, Mwana FA atakuwa ni kama msaidizi wa Waziri wa Sanaa, Utamaduni Na Michezo na uteuzi huo unakuja katika kipindi ambacho wasanii kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakitaka kuwepo kwa mwakilishi wao kwenye Wizara hiyo.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wasanii tofauti tofauti wa Tanzania wamempongeza MwanaFA kwa kushika nafasi hiyo. Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na AY, Barnaba Classic, Feza Kessy, Nandy, Billnass na wengineo wengi.

Leave your comment