Christina Shusho Atangaza Tarehe Ya Kuachia Album Yake Ya 'Hararat'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wakati wapenzi wa muziki wa Injili Tanzania wakiendelea kusubiri muziki mpya kutoka kwa Christina Shusho, nyota huyo wa muziki wa Injili hatimaye ametangaza tarehe ambayo anatarajia kuachia albamu hiyo.

Christina Shusho ambaye anajulikana kwa nyimbo kama Adamu, Mtetezi Wangu na Shusha Nyavu ametangaza tarehe ya kuachia albamu hiyo ikiwa ni takriban miezi mitatu tangu athibitishe kuwa ataachia albamu mwaka huu wa 2023.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shusho kupitia video fupi aliyoichapisha kwenye akaunti yake, amethibitisha kuwa albamu yake ya kuitwa Hararat itaingia sokoni April 9 mwaka huu wa 2023 akaenda mbali zaidi kwa kudokeza kuhusu eneo au ukumbi ambao uzinduzi huo utafanyika.

Ikumbukwe kuwa albamu ya Hararat imesheheni ngoma 25 ambazo ndani yake, Christina Shusho ambaye alitajwa kuwania tuzo za AFRIMMA mwaka 2022 ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Benjamin Weston, Anitha Musoki, Mercy Masika kutokea Kenya, Alarm Ministries kutokea Rwanda na wasanii wengine wa ndani na nje ya Tanzania

Leave your comment