Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Kusah Aturudisha Miaka Ya Nyuma Kwenye Ngoma Mpya "Wasi Wasi"
23 February 2023

[Picha: Screengrab/YouTube]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Msanii nguli kutokea nchini Tanzania, Kusah ameamua kukata kiu ya mashabiki zake kwa kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Wasi Wasi.
Kama moja ya wasanii hodari sana ndani ya Bongo Fleva kwenye suala la uandishi wa nyimbo, Kusah ameendelea kutetea nafasi yake hiyo kupitia mkwaju wake mpya wa kuitwa Wasiwasi ambayo ni ngoma yake ya kwanza kwa mwaka 2023
Kwenye Wasi Wasi Kusah anachukua vionjo vya muziki wa zamani kutengeneza ngoma nzuri ambayo ndani yake anahadithia namna ambavyo hamuamini mpenzi wake huku akidokeza kuwa anaogopa sana kuachwa. Utapenda kila kitu kwenye ngoma hii kuanzia mashahiri yake matamu mpaka mdundo wake ambao unatukumbusha enzi za Msondo Ngoma na Bendi Ya Sikinde.
Cukie Dady ndiye amehusika kutayarisha ngoma hii. Ikumbukwe kuwa, Kusah na Cukie Dady ameshirikiana pia kutengeneza nyimbo kama Karibu, On Fire pamoja na I Wish.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- The Marathon
25 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- TRUE LOVE
26 April
- O Daynor pisom 03 casou
24 April




Leave your comment