Alikiba 'Mahaba', Harmonize 'Single Again' Na Nyimbo Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Wiki hii ilikuwa ni wiki ya Bongo Fleva na muziki mzuri kwani wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania waliweza kupamba kiwanda cha muziki kwa ngoma mpya ambazo zina lengo la kuchangamsha mashabiki.

Kutoka kwa wasanii kama Ali Kiba, Harmonize, Micky Singer wengineo wengi hizi ndio ngoma bora kutoka Tanzania wiki hii :

Mahaba - Ali Kiba

Kinachofanya Mahaba Ya Ali Kiba kuwa bora sana ni mashahiri yake ambayo kama ulishawahi kuumizwa na mapenzi basi ujumbe wa Ali Kiba kwenye ngoma hii utakugusa na kukukosha sana. Mahaba imetayarishwa na Yogo Beatz na inafanya vizuri sana

https://www.youtube.com/watch?v=lDuxFGlm468

Wamelowa - Harmonize

Baada ya timu ya Simba kufungwa 3 na Raja CA siku ya Jumamosi, Harmonize aliamua kuwakera zaidi mashabiki wa timu hiyo kwa kuachia Wamelowa, ngoma ambayo inalenga kunanga na kutania mashabiki wa timu ya Simba, timu ambayo ina upinzani mkubwa na Yanga, timu ambayo Harmonize anaishabikia.

https://www.youtube.com/watch?v=zq5xowgBaTI

Nobody - Micky Singer

Katika harakati za kusherekea Valentine, Micky Singer aliamua kuachia Nobody, mkwaju mzuri wa mapenzi ambao ndani yake anahadithia mwanzo mwisho ni kwa namna anafurahi upendo na raha anazopewa na mwenzi wake

https://www.youtube.com/watch?v=mJyF41jn4-A

Single Again - Harmonize

Linapokuja suala la uandishi basi Harmonize hana mpinzani na kupitia ngoma yake hii ya Single Again, Harmonize amedhihirisha kuwa yeye ni mwandishi bora sana. Hii ni ngoma ya kwanza ya Harmonize kwa mwaka 2023.

https://www.youtube.com/watch?v=KT2E31at_n8

Unanisitiri Remix - Vanillah Ft Kayumba

Kama unatafuta ngoma ya kumpa shukran mpenzi wako ambaye alikuvumilia wakati unapitia changamoto basi usiache kusikiliza Remix hii ya Unanisitiri ambayo Vanillah amefanya na Kayumba kwani imeweza kufikisha aina hiyo ya ujumbe mahali pake.

https://www.youtube.com/watch?v=sBWqX6C2hGk

 

Leave your comment