Simba Sc Waangukia Pua, Yanga Sc Yang'ara- Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ile ahadi ya Rais Samia ya kutoa donge nono la fedha kwa kila goli litakalofunga na Simba au Yanga hatimaye imetimia baada ya timu ya Yanga kupokea kiasi cha Shilingi milioni kumi na tano kama ahadi kutoka kwa Rais Samia.

Wekundu wa Msimbazi Simba wao walishindwa kupata fedha hizo baada ya kupoteza alama tatu zingine Tena kutoka kwa Raja Casablanca kwa kufungwa mabao matatu kwa sifuri siku ya Jumamosi.

Simba waliutawala mpira zaidi ya Casablanca kwa asilimia 62 bila ya mafanikio ya kuona lango la wageni wao ambao wao walikuwa na asilimia 38 za umiliki wa mpira. Pia Kona 9 kwa Simba hazikuzaa matunda na upande wa Raja wakiwa na Kona 5.

Katika Mchezo huo kadi za njano tatu zilitolewa Simba wakiwa na Moja huku Casablanca wakiwa na kadi 2 za njano. Baada ya dakika 90 Simba wamebaki wakiburusa mkia katika mchezo wao wa pili ligi ya mabingwa Afrika wakipoteza michezo miwili mpaka sasa.

Kwa upande wao Yanga wao Jumapili hii ilikuwa njema sana kwa wapenzi wa klabu hiyo haswa baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza katika hatua ya makundi kombe la shirikisho. Licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake mahiri kama Bernard Morrison huku Aziz Stephan Ki akiingia katika kipindi Cha pili, Yanga Bado waliondoka na matokeo katika uwanja wa Mkapa.

Katika kipindi Cha kwanza pekee Wananchi walipachika mabao mawili ya mapema kutoka kwa Kennedy Musonda dakika ya 7 pamoja na Mudathir Yahya katika dakika ya 11 kabla ya kipindi Cha pili Tuisila Kisinda kapachika bao la tatu katika dakika ya 92.

Umiliki wa mpira kwa Yanga ulikuwa wa asilimia 51 kwa 49 walizokuwa nazo TP Mazembe huku Kona zikiwa 10 kwa Mazembe na Yanga waliambulia Kona tatu pekee.

Mashuti ya Moja kwa Moja yalikuwa 6 kwa kila timu huku pia kukiwa na kadi 2 za njano zilizotolewa mchezoni licha ya kutokea mashambi 13 kwa Wananchi na 11 kwa TP Mazembe.

Hii ni mechi ya pili kwa Yanga kuicheza katika hatua za makundi kombe la shirikisho na sasa wanashikilia nafasi ya pili katika kundi hilo.

Ahadi ya fedha za Rais Samia zilikabidhiwa mara baada tu ya mchezo wa Yanga dhidi ya TP Mazembe kukamilika huku Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt Pinda Chana akiongozana na Msemaji Mkuu wa serikali Greyson Msigwa walikabidhi fedha hizo.

Leave your comment