Nyimbo Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama unafuatilia kwa ukaribu muziki kutoka Tanzania huenda ukawa unajiuliza ni ngoma gani ambazo kwa sasa watanzania wanazisikiliza na kuzifuatilia sana nchini humo.  

Kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, Aslay na wengineo wengi hii hapa ni orodha ya ngoma 5 ambazo zinafanya vizuri nchini Tanzania kwa wiki hii kwenye mtandao wa Youtube :

Zuwena - Diamond Platnumz

Bongo Fleva safi iliyofanywa na Diamond Platnumz humu ndani ukichanganya na stori nzuri kuhusu Zuwena zimepamba sana ngoma hii ambayo ndani ya wiki mbili tu tangu kuachiwa kwake tayari imeshakusanya watazamaji takriban Milioni 7 Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=aOAjuAI0nJA&feature=youtu.be

Yatapita - Diamond Platnumz

Uhalisia ni kitu ambacho kimepelekea mashabiki wengi kuvutiwa sio tu na mashahiri bali na video pia ya Yatapita. Video ya Yatapita imefanyika hapa hapa nchini Tanzania maeneo ya Posta, Upanga na Ubungo Dar Es Salaam na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 11 Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=U6JBZNAkp24

Inauma - Aslay

Takriban wiki mbili tangu kuachiwa kwake lakini bado Inauma ya Aslay inaendelea kufanya vizuri Youtube. Huenda ni mashahiri au midondoko ya Aslay iliyovutia zaidi mashabiki kupenda kazi hii ya Aslay ambaye kwa sasa yupo chini ya Rockstar Africa

https://www.youtube.com/watch?v=-kK9O2B97HA

 

Utaniua - Zuchu

Zuhura Othman Soud aliamua kuchachua msimu huu wa Valentine na Utaniu, ngoma nzuri ya mapenzi ambayo kwa mara nyingine Imethibitisha kuwa linapokuja suala la uandishi Zuchu bila shaka anastahili kupewa heshima. Utaniua imeshasikilizwa takriban mara laki 6 Youtube

https://www.youtube.com/watch?v=e3erBs1myQo

 

Single Again - Harmonize

Harmonize amerudi tena na Single Again, ambayo ni ngoma yake ya kwanza mwaka huu. Ngoma hii imepokelewa vyema kabisa na mashabiki kwani ndani ya siku 3 imeshasikilizwa mara Milioni 1.3 Youtube

https://www.youtube.com/watch?v=KT2E31at_n8

 

Leave your comment