Ali Kiba Akosha Mashabiki Baada Ya Kudokeza Ngoma Yake Mpya "Mahaba"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Ali Kiba amerudisha tabasamu kwa mashabiki baada ya hivi kudokeza ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mahaba

Mshindi huyo WA tuzo ya MTV EMA kwa mwaka 2016 amedokeza kuhusu ujio wake mpya hivi karibuni na ngoma hiyo inayoshukiwa kuwa itaitwa Mahaba itakuwa ni ngoma ya kwanza kwa Ali Kiba kwa mwaka 2023.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ali Kiba alichapisha video akiwa sehemu inayofanana na jangwani akiwa na kipaza sauti anaimba ngoma hiyo ambayo kuanzia kionjo chake tu kinaonesha kuwa kimekosha mno mashabiki wa muziki ndani na nje ya Tanzania.

Tangu aachie albamu yake ya Only One King mwaka 2021, Ali Kiba amekuwa kimya na kwa mwaka jana, mfalme huyo wa Kings Music alitoa ngoma mbili tu ambazo ni Asali pamoja na Tile.

 
 
 
 
 
View this post on Instagram
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

A post shared by Alikiba (@officialalikiba)

Leave your comment