Vanillah Aachia 'Unanisitiri Remix' Akiwa Na Kayumba

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Akiwa kama moja ya wasanii wanaokuja kwa kasi sana kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Vanillah ameendelea kutikisa kiwanda cha Bongo Fleva na remix ya Unanisitiri ambayo akiwa amemshirikisha Kayumba.

Ujio wa remix hii ya Unanisitiri unakuja siku chache tangu Vanillah adokeze ujio wa ngoma hii ambayo wawili hawa yaani Kayumba na Vanillah wameweza kwa mara nyingine kuthibitisha umma kwamba wameiweka Bongo Fleva mikononi mwao.

Kwenye Unanisitiri Remix, Vanillah na Kayumba wanatoa shukran na sifa tele kwa wapenzi wao ambao wamekuwa wakiwavumilia na kuwasitiri bila kujali changamoto wanazopitia. Video ya ngoma hii imeakisi barabara maudhui ya ngoma nzima kwani imetengenezwa na stori yenye uhalisia.

Unanisitiri Remix ni ngoma ya tatu ambayo Vanillah ameshirikiana na msanii mwingine tangu aliposainiwa kwenye lebo ya Kings Music. Kufikia sasa ameshashirikiana na Tommy Flavour kwenye Whine For Me pamoja na K2ga kwenye Ananipigania.

https://www.youtube.com/watch?v=sBWqX6C2hGk

Leave your comment