Spurs Kuangukia Katika Mikono ya Tajiri Kutokea Iran - Mdundo Alt

[Picha: InsideSport.IN]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Bilionea kutokea nchini Iran mwenye asili ya Marekani Jahm Najafi anatarajiwa kuinunua klabu ya Tottenham Hotspur kwa kitita Cha Euro bilioni 3.1

Kwa mujibu wa gazeti la Financial times limesema tajiri huyo mwenye miaka 60 ambaye pia ni mmiliki wa kampuni  ya michezo ya MSP Sports Capital wako mbioni kuinunua Spurs kwa asilimia 70 huku asilimia 30 zilizobaki kutumiwa na wawekezaji wenza watakaokubali kushiriki katika mchakato huo wa umiliki

Kwa makadirio ya thamani ya klabu ya Tottenham Hotspur ni takribani Euro bilioni 2.5 pamoja na deni la timu hiyo linalokadiriwa kufikia Euro milioni 610 na kukamilisha thamani halisi ya timu hiyo.

Baada ya taarifa hiyo Najafi kwa sasa Yuko mbioni kuanza kutafuta na kuzungumza na wawekezaji wapya ambao watakamilisha asilimia 30 ya uwekezaji katika timu hiyo ya Tottenham Hotspur.

Sambamba na Hilo pia bado mazungumzo hayajafanyika kwa mnunuzi mpya wa timu hiyo pamoja na mmiliki wa timu hiyo bwana Joe Lewis pamoja na Mwenyekiti wa timu hiyo Daniel Levy yenye makazi yake katika viunga vya jiji la London huku mazungumzo yakitarajiwa kufanyika katika wiki za mbeleni.

Leave your comment