Simba, Yanga Washindwa Kung'ara Kimataifa - Mdundo Alt
16 February 2023
[Picha:Instagram]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Michuano ya kimataifa imeanza vibaya kwa Tanzania mara baada ya wawakilishi wao Simba na Yanga kupokea kichapo katika hatua za makundi Klabu bingwa Afrika pamoja na kombe la shirikisho Afrika.
Wakiwa nchini Guinea Simba Sports club walisafiri kwenda kukutana na Horoya AC ambako huko walipoteza kwa bao moja bila, goli lililofungwa na Pape Ndiaye katika dakika ya 18.
Katika kundi C ambalo Simba anashiriki ligi ya mabingwa Afrika Yuko katika nafasi ya 3 huku kundi hilo likiongozwa na Raja Casablanca wakifuatiwa na Horoya AC na Vipers SC wakiwa wanaburuza mkia.
Kwa upande wa wawakilishi wa Tanzania kombe la shirikisho, Young Africans sports club wao walishindwa kulinoa dafu katika dakika za mapema kabisa za mchezo mara baada ya kuwekwa mabao mawili ya ushindi dhidi ya US Monastir ya nchini Tunisia. Katika dakika ya 10, 16 Monastir walipata alama tatu katika kundi D kombe la shirikisho.
Mwanzo huu siyo mzuri kwa wawakilishi Hawa wa Tanzania labda yaweza kuwa mwanzo mgumu huku mechi zote zinazofuata watakutana na vinara wa makundi Yao hapo wiki ijayo
Kwa upande wa Simba baada ya mchezo huo pia walipendekeza mchezo wao unaofuata dhidi ya Raja Casablanca kuwe na mabadiliko ya muda lakini pendekezo Hilo limeshindikana kutokana na sababu ya kuwa mwenye maamuzi ya mwisho ni CAF na sasa Jumapili ya tarehe 18 Februari Simba watakutana na Raja Casablanca katika uwanja wa Mkapa.
Leave your comment