Lyrics: Zuchu - Unataniua

[Image Source: Instagram]

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Eti lah lah lah lalala lala lalaah

lah lah lah lalala lala lalaah

Nna hamu mwenzenu na hamu kuyahadithia

Oooh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia

 

Utani kama utani tulianza kimasihara

Sikudhani sikudhani yatafikia mahala

Akiwa hapatikani hapaliki sijalala

Kanifanya kitu gani mbona imekuwa mara

 

Dua kuku menipata mwewe wallahi nyinyi

Ni mtihani

Hata makosa afanye yeye mimi ndo naomba

Samahani

Ona anacheka kama mazuri

Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli

Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri

Na kwenye koma naweka nukta kanitia na kufuli

 

Oooh baby mimi hapa taabani

Wewe utaniua

Nimeoza dah yarabi sihemii

Wewe utaniua

Aaaah hizo raha zako

Wewe utaniua niua

Roho yangu mali yako

Wewe utaniua niua

 

Nikikosa stuli ni sunna kula kwenye mkeka

Unijue vizuri nikinuna mi ndo nadeka

Usije dhani kiburi uniache nikaja kuchekwa

Baby raha ya shughuli mkunwa awe nacheka heka

 

Oooh usichokipenda wewe

Chunga na mimi usinifanyie

Mgomba wangu mwenyewe eti ndizi nigombanie

Nipe penzi nilewe niyumbe nizimie

Oooh ringa kwangu upo mwenyewe kiboko yangu mie oooh vimba

 

Ona anacheka kama mazuri

Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli

Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri

Na kwenye koma naweka nukta kanitia na kufuli

 

Oooh baby mimi hapa taabani

Wewe utaniua

Nimeoza dah yarabi sihemii

Wewe utaniua

Aaaah hizo raha zako

Wewe utaniua niua

Roho yangu mali yako

Wewe utaniua niua

https://www.youtube.com/watch?v=e3erBs1myQo

 

Leave your comment