Free Download: Mwasiti, Kasolo na Rose Muhando Kwenye Nyimbo Mpya Ndani Ya Mdundo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wiki hii unasikiliza ngoma zipi? Kutoka hapa nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla baadhi ya wasanii wametoa ngoma kali na za kusisimua ambazo zina kila sababu ya kuwepo kwenye playlist yako siku ya leo.

Kutoka kwa wasanii kama Matonya, Mwasiti, Mwamposa na wengineo wengi, hizi hapa ni ngoma tano (5) ambazo unaweza kupakua bure on Mdundo na kuchangamsha playlist yako

Raha - Mwasiti

Mwasiti amerudi tena na Raha, ngoma ambayo ndani yake Mwasiti anahadithia namna ambavyo ametulia na kufurahi penzi analopewa na mpenzi wake. Humu ndani utapenda sauti tulivu ya Mwasiti pamoja na mashahiri ya aina yake ya Mwasiti

Piga Deki - Matonya

Matonya amerudi tena ngoma mpya ya kuitwa Piga Deki. Hii ni ngoma safi ya Bongo Fleva ambayo Matonya anajumuisha Bongo Fleva ya zamani pamoja na Bongo Fleva mambo sasa ili kuweza kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki.

Mwamposa - Sharara

Kama unapenda Amapiano basi hii ya kuitwa Mwamposa ya kwake Sharara ni kwa ajili yako. Humu ndani Sharara anazungumzia sifa za mtumishi aitwaye Mwamposa na namna ambavyo anashiriki kutatua changamoto za watu

Nimeipata Njia - Godwin Ombeni

Godwin Ombeni ameendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Injili na na katika ngoma yake hii mpya ya “Nimeipata Njia” Godwin Ombeni anashuhudia namna ambavyo maisha yake yamebadilika baada ya kupata njia ya uzima.

Inuka Uangaze - Stephen Kasolo & Rose Muhando

Kwenye Inuka Uangaze, Stephene Kasolo na Rose Muhando wanafuta machozi na kuwapa moyo watu waliokata tamaa kuwa wainuke na kuendelea kusonga mbele.

 

Leave your comment