Jinamizi Lazidi Kuitafuna Manchester City -Mdundo Alt

[Picha:The Times]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya timu ya soka ya Manchester City kukabiliwa na tuhuma za kuvunja sheria za kifedha katika ligi kuu ya Uingereza Kwenye makosa zaidi ya 100, sasa timu hiyo imetoa taarifa kulingana na jinamizi hilo linalowaandama kwa sasa.

Kwenye taarifa hiyo waliyoitoa City walisema ya kuwa

 " Manchester City FC imeshangazwa na kutolewa kwa madai haya ya ukiukaji wa Kanuni za Ligi Kuu, haswa kutokana na ushiriki mkubwa na mahitaji mengi ya kina ambayo EPL imepewa.

Klabu inakaribisha mapitio ya suala hili na Tume huru, kwa kuzingatia bila upendeleo mwili mpana wa ushahidi usiopingika ambao upo kuunga mkono msimamo wake.

Kwa hivyo tunatazamia jambo hili lisitishwe mara moja na kwa wote."

Tuhuma hizo zilizuka mara baada ya miaka minne ya uchunguzi katika klabu hiyo kwenye kipindi cha msimu wa mwaka 2008/2009 - 2017/2018 wakati kipindi kocha Roberto Mancini alipokuwa akiinoa timu hiyo.

Uchunguzi huo utachukua muda mrefu na endapo City watakutwa na hatia watalazimika kupatiwa adhabu kati ya zifuatazo, kulipa faini (fedha), kupunguziwa alama katika msimu husika wa ukweli utakapogundulika, kusimamishwa kucheza michezo ya ligi, kukataliwa au kusimamishwa kwa sajili za wachezaji na maamuzi mengine yatakayotewa.

Katika tuhuma hizo city wametuhumiwa kutumia fedha zaidi ya walichokuwa wakikiingiza na kuvunja sheria ya "fair play" kwa maana ya timu kutakiwa kuwa na uwiano sawa wa matumizi na kile timu inachokiingiza.

 

Leave your comment