Nyimbo Mpya Tanzania: Diamond Platnumz 'Zuwena' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwezi Februari umeanza vizuri sana kwa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kwani wasanii wengi kutoka Tanzania, wakubwa kwa wadogo wameachia ngoma mpya na kali zenye lengo la kufikisha mbali tasnia ya muziki nchini.

Hii ni wiki ambayo Diamond Platnumz ametukumbusha Bongo Fleva halisi, Joh Makini ameimba muziki wa Amapiano, Mavokali ametoa sifa kedekede kwa Yanga na mambo mengine mengi yametokea. Zifahamu ngoma mpya kutoka Tanzania wiki hii :

Zuwena - Diamond Platnumz

Diamond Platnumz ameturudisha kwenye Bongo Fleva kwenye Zuwena, ngoma ambayo imejaa mashahiri mazuri na ya kuvutia ambayo yanaelezea namna ambavyo binti aitwaye Zuwena alibadilika na kuanza kufuja mali mara baada ya mumewe kufariki.

https://www.youtube.com/watch?v=aOAjuAI0nJA

 

Wave - Joh Makini

Bila shaka Joh alikuwa Makini sana wakati anatayarisha ngoma hii ya Wave ambayo kwa sasa inasikika na kurindima kila kona ya Tanzania. Kwenye Wave, Joh Makini anapiga makasia kuzungumzia kuhusu umaarufu wa Amapiano nchini, hustles zake tangu aanze muziki na mambo mengine mengi sana

https://www.youtube.com/watch?v=wDIcIcMQdTY

 

My Baby - Diamond Platnumz

Diamond Platnumz ameamua kujing'arisha upya na My Baby ngoma ambayo anatoa sifa tele kwa mpenzi wake na kudokeza dhahiri shahiri ni kwa namna gani anampenda mpenzi wake huyo. Kwenye ngoma hii Diamond Platnumz anaonekana kuranda randa kwenye Bongo Fleva pamoja na Afrobeats.

Nakuja - Tommy Flavour Ft Marioo

Ili kutengeneza Nakuja Tommy Flavour aliomba usaidizi wa Marioo ambaye bila shaka amefanya mengi mazuri kwenye ngoma hii ambayo melody yake inatukumbusha ngoma ya Nioneshe ya Maua Sama akiwa na Ali Kiba

https://www.youtube.com/watch?v=UviYi2oqHos

Yanga Commando - Mavokali

Wiki hii Mavokali ameamua kuonesha mapenzi yake kwa Yanga kupitia ngoma hii ya kuitwa Yanga Commando ambayo imemlazimu yeye kusafiri mpaka Avic Town Kigamboni kwa ajili ya kuandaa video ya ngoma hii ambayo kufikia sasa inafanya vizuri sana Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=V3d1O0f77DY

Leave your comment