Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz Aachia Ngoma Mbili "Baby" Na "Zuwena"

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania Diamond Platnumz, Diamond Platnumz ameendelea kukoleza burudani kwa mashabiki zake na hii ni baada ya msanii huyo kuachia ngoma mbili siku ya leo yaani "Baby" na "Zuwena"

Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Yatapita ameachia ngoma hizo mbili yaani Baby na Zuwena ikiwa ni mara yake ya pili kufanya hivyo kwani mwaka 2014 mwezi Julai Diamond aliachia pia ngoma mbili kwa mpigo Bum Bum pamoja na Mdogo Mdogo.

Kwenye Zuwena Diamond Platnumz anarudi tena kwenye Bongo Fleva ambapo kwenye kibao hiki Diamond Platnumz anamzungumzia shemeji yake aitwaye Zuwena ambaye baada ya kurithi hela za mumewe anaamua kutumia pesa vibaya na kubadilisha mtindo wa maisha yake.

Kwenye ngoma hii sauti ya Diamond Platnumz inaonekana ikiwa imejaa huzuni, karaha pamoja majuto. Aidha kwenye ngoma hii pia Diamond Platnumz kwa mara nyingine tena anadhihirisha ufundi wake katika kuandika ngoma za Bongo Fleva kwani muda mwingi anatumia kiswahili sanifu.

Kwenye Baby, Diamond Platnumz anabadilika kidogo na kutuletea mtindo wa Afrobeats ambapo katika ngoma hii Diamond Platnumz anamsifia mpenzi wake na kukiri wazi jinsi gani anampenda mpenzi wake huyo.

Kwenye upande wa Video tayari Diamond Platnumz ameachia video ya Zuwena ambayo bila shaka imeakisi uhalisia wa ngoma nzima ya Zuwena. Video ya Zuwena imeongozwa na Director Ivan ambaye pia ameshafanya kazi na Diamond Platnumz kwenye Mtasubiri pamoja na Yatapita.

https://www.youtube.com/watch?v=aOAjuAI0nJA

Leave your comment