Yanga Yaendelea Na Ukimya Sakata La Sportpesa- Mdundo Alt

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya Yanga imeingia matatani mara baada wadhamini wakuu wa timu hiyo Sportpesa kuidai fidia pamoja na msamaha kutoka kwa Yanga kwa kile walichodai ni kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sportpesa imeeleza jinsi klabu ya Yanga ilivyoamua kuingia mkataba na kampuni nyingine kama wadhamini wakuu wa timu hiyo katika mashindano ya kombe la shirikisho wa Afrika.

Siku ya tarehe 30 Young Africans waliandaa hafla ya uzinduzi wa jezi pamoja na usainiwaji wa mkataba na kampuni ya Haier uliofanyika katika hoteli ya Serena.

Kwa mujibu wa Yanga katika hafla hiyo walimtaja Haier kama mdhamini Mkuu wa klabu hiyo katika mashindano ya kombe la shirikisho na kwa upande wao Sportpesa wamekanusha kutokuwa wadhamini wakuu wa timu hiyo ya Wananchi.

Katika taarifa waliyoitoa kwa umma Sportpesa waliwatuhumu Yanga kuuza haki miliki kwa kampuni ingine na waliandika ya kuwa " pendekezo letu lilikataliwa kwa kuwa klabu tayari ilikuwa imeuza haki hizi bila kujadili masharti ya kimkataba yaliyopo na Sportpesa"

Mpaka sasa klabu ya Yanga Bado haijatoa tamko lolote juu ya tuhuma hizo huku pia Sportpesa wakiwa wamepeleka barua kwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ikihusisha sakata hilo.

Kwa upande wake Meneja wa masuala ya kidigitali wa klabu ya Yanga Privaldnho kupitia ukurasa wake wa Twitter alipogusiwa kuhusiana na swala hilo alisema "Sasa masuala ya mkataba mimi naongeleaje? Naweza kujibu maandiko yenu ninyi ila siyo mikataba ya klabu.."

Leave your comment