Wasanii Kutoka Tanzania Wanaotarajia Kuachia Ngoma Kipindi Cha Valentine

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msimu wa Valentine unakaribia na wasanii wengi kutoka nchini Tanzania tayari wameshaahidi kuachia ngoma, Albamu na hata EP kwa ajili ya kipindi hiki ambacho wapendanao watakuwa wanasherehekea na kukumbushana mengi.

Wafuatao ni wasanii kutoka Tanzania wanaotarajia kuachia ngoma katika kipindi hiki cha Valentine

Rayvanny

Februari ni mwezi ambao Rayvanny kwa kawaida huachia mfululizo wa Flowers EP na kwa mwaka huu wa 2023 msanii huyo tayari ametangaza kuachia Flowers III kama zawadi kwa mashabiki kipindi cha Valentine.

Siku chache zilizopita kupitia uwanja wake wa Instastory Rayvanny alidokeza ujio wa Flowers III na hivyo kuwaweka mashabiki chonjo kuhusu ujio wake huo mpya. Kufikia sasa bado Rayvanny hajatangaza orodha ya ngoma wala wasanii walioshirikishwa kwenye kazi yake hiyo.

https://www.youtube.com/watch?v=DyHnyHQx2vs

Linex

Hivi karibuni Linex ametangaza kuwa ifikapo Februari 14 mwaka huu ataachia EP yake yenye ngoma 3 ya kuitwa 3 Za Mjeda 2.

Kando na Valentine, tarehe hiyo ya Februari 14 pia Linex atakuwa anatimiza mwaka mwingine kwenye maisha yake na hivyo kutengeneza hari zaidi kwa mashabiki kusikiliza EP hiyo ya kuitwa 3 Za Mjeda 2.

https://www.youtube.com/watch?v=8AcH8NRiMho

Maua Sama

Maua Sama anatarajia kuachia albamu yake ya kwanza tangu aanze muziki tarehe 14 Februari mwaka huu, albamu ya kuitwa Love Waves na kufikia sasa, Sama ambaye alitetemesha Tanzania miaka kadhaa nyuma na Iokote, tayari ameshatoa mkwaju mmoja wa kuitwa Mr. DJ.

https://www.youtube.com/watch?v=nYoWChyv4h0

 

Kwa sasa Mr DJ inafanya vizuri sana sehemu tofauti na pasi na shaka ifikapo Februari 14 mashabiki watapata muziki mzuri kutoka kwa Sama ambaye kipaji kwa mara ya kwanza kiliaminiwa na rapa MwanaFA.

Leave your comment