Diamond Atangaza Kusaini Msanii Mpya WCB Wasafi

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Wakati ngoma yake ya Yatapita ikiendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania, mwanamuziki nguli kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameingia kwenye vichwa vya habari nchini baada ya kutangaza kwamba tayari amesaini msanii mpya kwenye lebo yake ya WCB Wasafi.

Diamond Platnumz ambaye mwaka jana aliibuka kama msanii bora Afrika Mashariki  kwenye tuzo za Headies ametangaza kwamba ameongeza msanii mwingine kwenye leob yake ya WCB Wasafi. Taarifa hii inakuja siku chache tangu Nandy atambulishe msanii wake mpya wa kuitwa Yammi.

Kupitia Instastory yake, Diamond Platnumz ameonesha kipande kidogo cha mkataba cha msanii wake huyo ambapo kwenye mkataba huo inaoneshwa kwamba msanii huyo amesaini mkataba huo siku ya leo Februari 2 mwaka 2023. Kufikia sasa Diamond Platnumz hajamtaja msanii wake huyo mpya ambaye watanzania wanamsubiri kwa hamu sana.

[Picha: Diamond Planumz/Instagram]

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho kwa Diamond Platnumz kusaini msanii mpya ilikuwa ni mwaka 2020 baada ya kumtambulisha Zuchu na tangu hapo kufikia sasa hajatangaza msanii mwingine yoyote kwenye lebo hiyo kubwa Afrika Mashariki.

https://www.youtube.com/watch?v=U6JBZNAkp24

Leave your comment