Video 5 Za Muziki Kutoka Kwa Harmonize Zilizozua Gumzo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Tangu atambulishwe kama msanii wa Wasafi mwaka 2015, Harmonize siku zote amekuwa ni habari. Kupitia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na katika mazungumzo ya wapenda muziki mtaani Harmonize amekuwa ni mada isiyoisha.

Kuanzia maisha yake, muziki wake, mahusiano, kauli zake na hata kikohozi chake ambacho kilipamba vyema ngoma tofauti tofauti kama Woman ya Otile Brown, Champion Remix ya Kontawa na nyinginezo nyingi, ni wazi kwamba Harmonize siku zote amekuwepo.

Moja kati ya sehemu ambazo wengi wamekuwa wakimzungumzia Harmonize ni kwenye video zake za muziki ambazo kwa namna moja au nyingine zimekuwa zikizua gumzo hasa kutokana na wahusika wanaotumika au stori ya video kwa ujumla  kuwa na ukakasi.

Zifuatazo ni video 5 kutoka kwa Harmonize ambazo zilizungumziwa sana pindi zilipotoka :

Niambie

Ili kuiandaa Niambie, Harmonize alikwea pipa mpaka Afrika Kusini na ndani ya video hii Harmonize anamtumia mwigizaji Jackline Wolper kama model.

Wakati video hii inatoka Harmonize alikuwa kwenye mahusiano na mwigizaji Jackline Wolper na kitendo cha Harmonize  kumshirikisha Wolper kwenye video ambaye kwa kipindi kile alikuwa mpenzi wake kilichagiza wengi kuizungumzia video hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 21 huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=Jihz0uX3XOo

Wote

Wote ni ngoma namba 4 kwenye albamu ya Harmonize ya kuitwa "Made For Us" na hivi karibuni Harmonize aliachia video ya ngoma hiyo akiwa amemshirikisha mwanamuziki Feza Kessy.

Kabla ya video hii kuachiwa, Harmonize alichapisha picha akiwa na Feza Kessy ufukweni kitu kilichosababisha wengi kudhani kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano na hata video ilivyotoka wengi waliisifia kutokana na uigizaji wa wawili hao kwenye video kuleta uhalisia sana huku wengi wakishuku kuwa huenda wawili hao walikuwa wapo kwenye mahusiano.

https://www.youtube.com/watch?v=NVOuH9vDCXI

Ushamba

Kwenye Ushamba, Harmonize kwa mara nyingine aliingia midomoni mwa watu na hii ni baada ya kumshirikisha mtu kwenye video ambaye alikuwa anafanana sana na Diamond Platnumz ambaye ni bosi wake wa zamani.

Kwenye video ya Ushamba mtu ambaye wengi walitaja kwamba anafanana na Diamond Platnumz anaonekana akipiga picha kwenye swimming pool, kipande ambacho kilisababisha gumzo na mazungumzo makubwa mtandaoni kiasi cha Director Hanscana kujitokeza na kutoa maelezo akiwa kwenye interview na Simulizi na Sauti.

https://www.youtube.com/watch?v=sZ420sDOumE

Amelowa

Muda mfupi baada ya Kajala na Harmonize kutangaza kuachana kwao, wengi walianza  kumtaja vixen wa kwenye Amelowa wa kuitwa Sophie ambapo wengi walimtaja Sophie kama chanzo cha achano lao, kitu ambacho mpaka leo si Harmonize wala Kajala alishawahi kuthibitisha.

Tangu Amelowa imetoka, Sophie amekuwa akipata interviews nyingi kwenye vyombo vya habari

https://www.youtube.com/watch?v=-HZZ6vs_dfQ

Mdomo

Video ya Mdomo ya kwake Harmonize akiwa amemshirikisha iliweka rekodi mpya ya duniani baada ya kufikisha watazamaji Milioni 1.3 ndani ya dakika tatu tu. Rekodi hii iliwashangaza watu wengi ambao walionekana kutoamini rekodi hiyo.

https://www.youtube.com/watch?v=b07caYNoBXQ

Leave your comment