Foby Ajuta Baada Ya Kupokea  Ujumbe Wa Msanii, Ne-yo Wa Marekani

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka Tanzania, Foby hivi karibuni ameonesha kujutia baada ya kushindwa kujibu ujumbe wa Instagram yaani DM kutoka kwa msanii wa Marekani, Neyo.

Foby ambaye alitikisa Tanzania na ngoma yake ya Emoji wiki kadhaa nyuma amedokeza hivi karibuni kuhusu DM aliyoipa ta kutoka kwa msanii wa Marekani Neyo. Foby ni msanii kutoka Tanzania ambaye alipata umaarufu miaka kadhaa nyuma baada ya kuachia ngoma ya Star na tangu hapo amekuwa akijitengenezea nafasi kwenye Bongo Fleva kila kukicha.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, hivi karibuni Foby kwenye Instastory alionesha screenshot ya ujumbe aliotumiwa na msanii Neyo kutoka Marekani takriban wiki 20 nyuma lakini hakuona hivyo hakujibu na kisha kuwashauri wasanii wengine kuwa kuna umuhimu wa kusoma emails na kuangalia DM kipindi wakitoa ngoma

"Hakuna kitu Muhimu Kwa msanii kwa sasa kama kupekua DM na Emails hasa unapoachia Project Mpya Pekua mpaka chini huko mana DM na emails za pongezi huwa nyingi Mno!! Dah?? Hii imeniuma sana!! Sijui hata kama atareply nikimtext sahivi na ma wiki 20 yamepita babekiii!!" aliandika msanii huyo.

Ikumbukwe kuwa Neyo ni msanii mkubwa wa R&B kutoka Marekani ambaye pia alishafanya kazi na Diamond Platnumz kwenye ngoma ya Marry You ambayo ilifanya vizuri sana ndani na nje ya Tanzania.

Leave your comment