Lyrics: Aslay- Inauma

[Image Source: Instagram]

Pakua na Kuskiza mziki wa Yammi Tz Ndani Ya Mdundo

Tuna siku tatu toka tumeachana

Yaani juzi kuamkia jana

Yaani hata week haijaisha

kinachonisikitisha tayari ameshapata bwana

 

Halafu hawazi

Haonyeshi dalili ya machozi

Yaani bonge la surprise amenifanyia

Mwili wote umeingiwa ganzi

Ina maana alikuwa ananisaliti

Ndiyo maana haikupita hata week

Inauma maumivu hayasimuliki

kuona wakipeti peti hadharani

 

Wanajua kunirusha roho

wakiniona ndiyo wanashikana

Malove bite kwenye shingo

kwa mdomo ndiyo wanalishana

 

Yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Najikaza kisabuni lakini roho inauma

yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh Yala weeh inauma

Najikaza najikaza lakini ukweli inauma

Yala weeh yala weeh inauma

 

Aiyooooo

lile lile

Aaaah lilele eeh

 

Jamani mi ndugu yenu ninateseka

Nitahama nivikimbie hivi vibweka

Majirani nao washaanza kunicheka

Nyimbo za mafumbo ameachwa ameachwa

 

Akili inanituma nikapigane

Ila mwana mbavu kajazia simuwezi

Natamani nimtukane

Ila nikimuona nabaki kigugumizi

 

Naomba wafe baharini waliwe na papa

Halafu yule papa avuliwe aletwe hapa

Nimle nishibe na miba niwape paka

Wivu umenishika nimechoka nimechoka

 

Wanajua kunirusha roho

Wakiniona ndiyo wanashikana

ma love bite kwenye shingo

Kwa mdomo ndiyo wanalishana

 

Yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Najikaza kisabuni lakini roho inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Yala weeh yala weeh inauma

Najikaza najikaza lakini ukweli inauma

Yala weeh yala weeh inauma

 

Nasikia wivu

Inamaana magetoni ndiyo haji tena

Mwenzenu Nasikia wivu

Alivyonipa mimi anampa yule bwana

Nasikia wivu

Ooh inauma

 

Mwenzenu nasikia wivu

Jamani eeh inauma

Nasikia wivu

Inauma

Mwenzenu nasikia wivu

 

Nasikia nasikia

Nasikia wivu

Eeeh lele

Mwenzenu Nasikia wivu

Unaniumiza wivu

Leave your comment