Nyimbo Mpya: Maua Sama Amnanga Ex Wake Kwenye  Ngoma Mpya "Mr Dj"

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Maua Sama Ndani Ya Mdundo

Fundi wa R&B kutoka Tanzania, Maua Sama ameendelea kuwasha moto kwenye kiwanda cha Bongo Fleva na hii ni baada ya kuachia ngoma yake mpya ya kuitwa Mr DJ.

Hivi karibuni Maua Sama alitangaza kuachia albamu yake ya Love Waves ambayo itaingia sokoni Tarehe 14 Februari. Kulingana na Maua Sama Mr DJ ndio ngoma ya kwanza kuiachia kutoka kwenye albamu ya hiyo ambayo inasubiriwa sana na mashabiki.

Kinachofanya ngoma ya Mr DJ kuwa bora sana ni ujumbe na maudhui ya ngoma kwa ujumla. Kwenye ngoma hii, Maua Sama anaringa kwa sababu ya raha anayoipata kwenye mahusiano yake mapya. Humu ndani Maua Sama anatupa vijembe and maneno ya kejeli kwa mpenzi wake wa zamani.

Ngoma Ya Mr DJ imetayarishwa na Alien Traxx, imeandikwa na msanii Micky Singer huku maandalizi ya mwisho yaani Mixing and Mastering yakiwa yameshughulikiwa na Lizer Classic kutokea Wasafi Records.

https://www.youtube.com/watch?v=nYoWChyv4h0

Leave your comment