Ubashiri Mechi ya Manchester City Vs Arsenal - Mdundo Alt

[Picha:Arsenal Mania]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kuelekea mzunguko wa 4 wa kombe la FA Manchester City wanakwenda kuwa wenyeji wa Arsenal mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Etihad siku ya Ijumaa.

Katika mchezo huo City wanaingia wakiwa kifua mbele baada ya kuwafunga Arsenal katika michezo mitano ya mwisho waliyokutana licha ya wao kuwa katika nafasi ya pili katika ligi na Arsenal wakiwa wanaongoza ligi.

Kwa kiwango cha The Gunners msimu huu wakiwa chini ya Mikel Arteta wana uwezo mkubwa zaidi wa kupindua historia na kurudisha heshima dhidi ya Man city katika mchezo huo.

Pep Guardiola huu unaweza usiwe mchezo wenye umuhimu kwake baada ya kauli yake aliyoitoa katika mchezo dhidi ya Manchester United ya kuhitaji vikombe vikubwa zaidi kwa maana ya kombe la mabingwa ulaya kutokana na kuwa na vikombe vyote vya ndani akiwa  kama meneja wa timu hiyo.

Manchester city kwa sasa hawana majeruhi na hivyo katika mchezo huu Pep anauwezo wa kufanya uchaguzi wowote kwa wachezaji atakaoona wanaweza kumpatia matokeo.

Kwa Arsenal wao wana majeruhi watatu akiwemo mshambuliaji Gabriel Jesus, kiungo Mohamed Elneny pamoja na winga Reiss Nelson.

Odds za Manchester city kushinda mchezo huu au kutoa sare ni 1.26.

Leave your comment