Diamond Platnumz Agusa Hisia  Za Wengi Kwenye Video Mpya Ya "Yatapita"

[Picha: Screengrab/YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Vanilla Ndani Ya Mdundo

Wakati wana Afrika Mashariki wanaendelea kurahani na kuimeng'enya vizuri ngoma ya Yatapita, CEO wa WCB Diamond Platnumz hivi karibuni amenogesha zaidi mradi huo kwa kuachia video ya ngoma hiyo ambayo imegusa hisia za watu wengi.

Diamond Platnumz ambaye hivi karibuni ametajwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za Soundcity MVP tayari ameachia Video Ya Yatapita ambayo wengi walikuwa wanaisubiri kwa hamu. Video ya Yatapita ni video ya kwanza kutoka kwa Diamond Platnumz kwa mwaka huu wa 2023.

Video ya Yatapita imeakisi vyema ujumbe na mashahiri ya ngoma ya ngoma yenyewe kwani ndani ya video, Diamond Platnumz anachukua uhusika wa mwanaume ambaye  hana kipato kikubwa na hivyo anampa faraja na tumaini mpenzi wake kuwa mambo yote hayo Yatapita. Kwenye video Diamond Platnumz anaonekana akinyanyaswa kwenye eneo la kazi, akiishi kwenye mazingira mabovu na kupitia changamoto mbalimbali na mpenzi wake.

Moja ya kipande ambacho kimegusa hisia za, wengi ni pale ambapo Diamond Platnumz na mpenziwe wanaonekana wakiwa wanaandaa  chakula na baada ya kumaliza wakiwa wanakaribia kuanza kula mboga walivyokuwa wameiandaa inaliwa huku wakiwa wamebaki kwenye bumbuazi.

Director Ivan ndiye muandaaji wa video hii ambayo watu wengi wameonekana kuipenda na kuisifia kwani Diamond Platnumz amegusia maisha ya mtanzania wa kawaida. Director Ivan pia ndiye aliandaa video ya Mtasubiri ya Diamond Platnumz, Utu ya Ali Kiba, Wote ya Harmonize pamoja na Nitongoze ya Rayvanny.

https://www.youtube.com/watch?v=U6JBZNAkp24

Leave your comment