Wasanii Watano Wanaotarajia Kuachia Albamu / Ep Mwaka 2023

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Vanilla Ndani Ya Mdundo

Wapenzi wa muziki kutoka Tanzania wana mengi ya kutegemea kwa mwaka huu wa 2023 ikiwemo baadhi ya wasanii wakubwa kuachia Albamu Na EP. Kupitia mitandao ya kijamii na mazungumzo na vyombo vya habari kuna baadhi ya wasanii kwa nyakati tofauti tofauti walidokeza kuhusu ujio wa albamu kwa mwaka huu.

Wafuatao ni wasanii kutoka Tanzania ambao wanatarajiwa kuachia albamu / EP  mwaka huu wa 2023:

Q Chief

Q Chief alishangazwa wengi hivi karibuni baada ya kutangaza kuwa kwa mwaka huu ataachia albamu tatu, kauli aliyoitoa kupitia akaunti yake ya Instagram. Aidha Q Chief aliongeza kwa kusema kuwa ataanza kwa kutoa albamu yake ya The Last Meal Januari hii.

Maua Sama

Mapema mwaka huu kupitia akaunti yake ya Instagram, Maua Sama alidokeza kuwa Terehe 14/02 ataachia albamu yake ya kuitwa Love Waves. Hii ni albamu ya kwanza ya Maua Sama tangu aanze muziki na inakuja miezi michache tangu aachie EP yake ya kuitwa Sinema.

G Nako.

Baada ya kuidokeza kwa muda mrefu, hatimaye G Nako hivi karibuni amedokeza kwamba EP yake itatoka Februari 3 mwaka huu na itaitwa Make You Dance. Kwenye EP yake hiyo G Nako ameandaa ngoma 6 ambazo ameshirikisha wasanii kama Rayvanny pamoja na Dreygon

Christina Shusho

Baada ya kukaa takriban miaka minne bila kutoa album, Christina Shusho hivi karibuni ametangaza kurudi na albamu mpya inayoitwa Hararat. Hararat ni albamu yenye ngoma 25 na ndani yake ameshirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Benjamin Weston, Mercy Masika, Anitha Musoki na wengineo wengi.

Zuchu

Malkia kutoka WCB, Zuchu kwa muda mrefu sasa amekuwa akidokeza kuhusu albamu yake. Akiongea na Refresh miezi kadhaa nyuma, Zuchu alisema kwamba yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya albamu hiyo na kwamba kuna baadhi ya wasanii aliowashirikisha walikuwa bado hawajamaliza kurekodi vipande vyao.

 

Leave your comment