Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz 'Yatapita', Lady JayDee 'I Found Love' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Januari umekuwa ni mwezi mwingine mzuri kwenye kiwanda cha Bongo Fleva na hii ni kutokana na wasanii kutoka Tanzania kuachia ngoma kali ambazo bila shaka zimekonga hisia za mashabiki mbalimbali wa muziki.

Kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, Ibraah, Nay Wa Mitego na wengine wengi hizi ni baadhi ya ngoma bora kutoka Tanzania wiki hii

Yatapita - Diamond Platnumz

Baada ya kutembea kwenyr Amapiano na Afrobeats kwa muda kidogo, wiki hii Diamond Platnumz amerudi kwenye ngome ya Bongo Fleva na Yatapita, ngoma ambayo Diamond Platnumz amelenga kuwapa moyo wanaume wote watafutaji ambao wana wapenzi. Mdundo wa Yatapita umetayarishwa na Lizer Classic na kwa sasa mashabiki wanasubiri video ya ngoma hiyo kwa hamu sana.

https://www.youtube.com/watch?v=FAZs7oRhGiQ

Tunapendeza - Ibraah Ft Harmonize

Ibraah na Harmonize wamerudi tena na Amapiano kali ya kuitwa Tunapendeza ikiwa ni ngoma ya kwanza ya Ibraah tangu aachie "King Of New School". Tunapendeza imeundwa kwa beat kali lakini kinachonogesha zaidi ngoma hii ni mashahiri mazuri ya Harmonize na Ibraah ambayo yamepangiliwa vizuri.

https://www.youtube.com/watch?v=olzi1dFC5H4

3 Hearts EP - Yammi

Kutoka kwenye lebo ya The African Princess, msanii Yammi ambaye ametambulishwa hivi karibuni na Nandy ameachia EP yake ya 3 Hearts. Kwenye ngoma hizi tatu Yammi anapambanua uwezo wake wa kuimba Baibuda na utapenda namna ambavyo ameimba kuhusu raha, karaha na maumivu yanayotokana na mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=DwKka8oNiL0

 

I Found Love - Lady Jaydee & Rama Dee

Baada ya Suluhu na Matozo, Lady Jaydee na Rama Dee kwa mara nyingine wamechachua kiwanda cha Bongo Fleva kwa kuachia I Found Love. Ngoma hii nzuri ya mapenzi ambayo imetayarishwa na Motion Beatz, imeandikwa na G Boy huku video ikiwa imeandaliwa na Nicklass

https://www.youtube.com/watch?v=XhVwmbdIDhg

 

Nakuja - Nay Wa Mitego Ft Phina

Ili kutengeneza Nakuja Nay Wa Mitego aliamua kugawana kipaza sauti na Phina na bila shaka wameweza kuleta ngoma kali ya mapenzi ambayo imepambwa na michano mikali ya Nay Wa Mitego pamoja na sauti ya ndege mnana ya kwake Phina.

https://www.youtube.com/watch?v=qFie5W_oKYk

 

Leave your comment