Robertinho Aondoka Simba SC Kwa Muda- Mdundo Alt

[Picha: Sports News Africa]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC Roberto Oliviera, amefungasha virago vyake na kuelekea nchini kwao Brazil siku ya jana baada ya mechi ya Simba dhidi ya Dodoma Jiji, mechi iliyoisha kwa Simba kushinda bao 1-0.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti limeeleza sababu za kuondoka kwa Robertinho kuwa ni kuisha kwa muda wa pasipoti yake ya kusafiria, hivyo kulazimika kurudi Brazil ili kufuatilia taratibu za pasipoti kutokana na kutokuwa na ubalozi wa Brazil nchini Tanzania.

Kuondoka kwa Robertinho kunamuachia majukumu mzawa Juma Mgunda ambaye amejiwekea Imani katika klabu hiyo kutokana na jinsi alivyoiendesha Simba kwa miezi kadhaa hapo nyuma, na atashirikiana na makocha wengine pamoja na benchi zima la ufundi

Mbrazili  Robertinho ataukosa mchezo wa kombe la shirikisho ambapo Simba watavaana na Coastal Union ya Tanga hapo mbeleni.

Safari hiyo ya kurejea Brazil, ni moja kati ya maandalizi ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika itakayoanza mwezi  Februari na kujiepusha na vikwazo wakati wa safari za michuano hiyo.

Leave your comment