Lampard Atimuliwa Everton- Mdundo Alt

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kocha wa klabu ya Everton Frank Lampard amefutwa kazi hapo jana kutokana na mwenendo mbaya wa klabu hiyo tangu kuanza kwa ligi. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii pamoja na website Everton imetoa taarifa ya kumfuta kazi kiungo huyo wa zamani wa Chelsea.

Lampard ambaye alijiunga na Everton mwaka jana amedumu klabuni hapo kwa muda wa miezi 12 tu mpaka kufukuzwa kwake kazi.

Msimu uliopita wa mwaka 2021-2022 timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 16 na kwa sasa ikiwa katika nafasi ya 19 huku kukiwa na hatari ya kushuka daraja.

Kwa msimu wa mwaka 2022-2023 timu hiyo imefanikiwa kushinda mechi tatu na kutoa sare michezo sita lakini pia Everton imepoteza jumla ya michezo 11 kati ya michezo 20 waliyoicheza msimu huu mpaka sasa.

Kutokana na hali mbaya ya The toffees wako katika wakati mgumu wa kugeuza meza na kupata matokeo hasa wakati huu ikiwa Bado inatafuta meneja mpya pamoja na makocha wapya.

Mbali na Lampard uongozi wa Everton pia umewatimua wafanyakazi wengine wa benchi la ufundi na kumuacha kocha wa walinda mlango Alan Kelly pekee huku waliofutwa vibarua wengine ni pamoja na kocha msaidizi Joe Edwards, Paul Clement, pamoja na kocha wa viungo Chris Jones.

Leave your comment