Wasanii Wa Tanzania Waliotajwa  Kuwania Tuzo Za Soundcity Mvp Awards 2023

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kiwanda cha muziki nchini Tanzania kimezidi kunawiri na kuongeza ushawishi Afrika baada ya hivi karibuni wasanii kutoka Tanzania kutajwa kuwania tuzo za Soundcity MVP kwa mwaka huu wa 2023.

Tuzo za Soundcity MVP Awards huandaliwa na kituo cha Radio na TV cha huko nchini Nigeria kwa lengo la kuheshimisha wasanii wanaofanya vizuri zaidi kwenye muziki na kwa mwaka huu tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika huko nchini Nigeria tarehe 11 Februari.

Kutoka nchini Tanzania, Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele 5 kama Msanii Bora Upande Wa Digital, Chaguo La Wasikilizaji (Listener's Choice), Video Bora Ya Mwaka, Msanii Bora Wa Kiume na Msanii Bora Wa Mwaka.

Zuchu ni msanii mwingine ambaye ametajwa kuwania tuzo hizo ambapo ametajwa kuwania kipengele cha Msanii Bora Mwaka, Msanii Bora Wa Kike, Video Bora Ya Mwaka Na Msanii Bora Upande Wa Digital.

Msanii Phina ambaye aliiteka Tanzania mwaka 2022 na ngoma yake ya Upo Nyonyo ametajwa kuwania kipengele cha Msanii bora Chipukizi akiwa anachuana vikali na Black Sheriff, Ayra Starr, Fave na wengineo wengi.

Ngoma ya Kwikwi ya Zuchu imempatia mtayarishaji wa muziki S2kizzy kuwania kipengele cha Mtayarishaji Bora Wa Muziki Afrika.

Leave your comment