Nyimbo Mpya: Ibraah Aachia Ngoma Mpya 'Tunapendeza' Ft Harmonize

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutokea Konde Music Worldwide, Ibraah hivi karibuni ameamua kukosha mashabiki zake baada ya kuachia kibao kipya kabisa cha kuitwa Tunapendeza ambacho ndani yake amemshirikisha Harmonize.

Tunapendeza ni ngoma ya kwanza ya Ibraah kwa mwaka 2023 na mradi wake wa kwanza tangu aachie albamu yake ya King Of New School mwaka 2023. Ngoma hii pia inakuja siku chache tangu Harmonize adokeze ujio wake kupitia Instastory.

Kwenye Tunapendeza Ibraah anaamua kudandia mdundo wa Amapiano ambapo Ibraah anaeleza kwa kina ni kwa namna gani anampenda na kujivunia mpenzi kiasi cha kushindwa kuishi kisa mpenzi wake huyo. Ngoma hii ni moja ya Amapiano chache Tanzania ambazo zimetungwa kwa mashahiri mazuri huku mpangilio wa sauti baina ya Harmonize na Ibraah ukiwa maridadi sana.

Kabla ya ngoma hii, Ibraah na Harmonize pia walishawahi kushirikiana kwenye ngoma mbalimbali kama One Night Stand pamoja Mdomo pamoja na Addiction ngoma pia ilifanya vizuri sana ndani na nje ya nchi.

https://www.youtube.com/watch?v=olzi1dFC5H4

Leave your comment

Top stories

More News