Nandy Atambulisha Rasmi Msanii Wa Kwanza Wa The African Princess Label

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki na msanii maarufu kutoka nchini Tanzania, Nandy hivi karibuni ametambulishwa msanii wa kwanza wa kwenye leob yake YA The African Princess ambayo ameizindua hivi karibuni.

Nandy ambaye ni mshindi wa tuzo za AFRIMMA amemtambulisha Yammi kama msanii wa kwanza wa The African Princess katika hafla ambayo ilivuta umakini wa vyombo vingi vya habari Tanzania. Ikumbukwe kuwa lebo ya Nandy, The African Princess imejikita zaidi kusimamia wasanii wa kike sio tu wa Tanzania bali Afrika kwa ujumla.

Pamoja na kutambulishwa kwake Yammi pia ameachia EP yake ya kuitwa 3 Hearts ambayo ndani yake imesheheni ngoma tatu ambazo ni Namchukia, Tunapendezana na Hanipendi. Hii ni EP ya kwanza kutoka kwa Yammi na inatarajiwa kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

Kutoka kwenye EP yake hiyo ya 3 Hearts, Yammi ameweza kuimba muziki aina ya Baibuda ambapo katika nyimbo zake zote hizo ameweza kuzungumzia kuhusu maumivu ya mapenzi na mahusiano kwa ujumla.

https://www.youtube.com/watch?v=W0RZZG63iB8

 

Leave your comment

Top stories

More News