Simba SC Yaajiri Kocha Mpya Ouanane Sellami- Mdundo Alt

[Picha: Simba Fc /Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka ya Simba Sc kutokea Tanzania imekamilisha taratibu zote na kumwajiri kocha msaidizi Ouanane Sellami (42) mwenye asili ya Tunisia.

Ujio wa kocha huyo kumetajwa kuwa moja katii ya mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo Robertinho ambaye pia ameonesha kuwa na mikakati ya kimageuzi katika klabu hiyo ya wekundu wa msimbazi.

Kabla ya kujiunga na wekundu wa Msimbazi Sellami mwenye liseni ya daraja B (CAF) amefanikiwa kufundisha vilabu kama vile Almadina ya Libya pamoja na Gabesien kutokea nchini Tunisia.

Hapo awali nafasi hiyo ya kocha msaidizi wa klabu hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Juma Mgunda ambaye  pia alikuwa kocha mkuu wa muda wa timu hiyo baada ya Simba kuvunja mkataba wake na kocha wa kipindi hicho mhispania Pablo Martin.

Kwa mujibu wa Simba, kocha huyo atasaidia maboresha zaidi katika benchi la ufundi haswa katika michuano ya ndani  pamoja na ile ya nje ya klabu hiyo akishirikiana na Juma Mgunda pamoja na Selemani Matola.

Baada ya utambulisho wa Sellami baadhi ya mashabiki wa klabu ya Simba wameonesha kutokuridhishwa na ujio wa kocha huyo kupitia maoni waliyoyaandika katika kurasa za mitandao ya kijamii za Simba, wakionesha kuwa na imani zaidi na kocha Juma Mgunda.

Leave your comment