Belle 9 Afunguka Sakata La Wasanii Wakubwa Kuhusishwa Kujiunga Wcb Wasafi
13 January 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Nyota wa muziki Tanzania Belle 9 hivi karibuni amefunguka kuhusu suala la wasanii wakubwa Tanzania kuhusishwa na kujiunga na lebo inayomilikiwa na Diamond Platnumz, WCB Wasafi.
Belle 9 ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Watu, hivi karibuni ametoa mawazo yake kuhusu namna ambavyo wasanii wakubwa nchini Tanzania wanahusishwa kujiunga na WCB Wasafi, ambayo ni moja ya lebo kubwa barani Afrika kwa sasa.
Akiwa kwenye mahojiano katika kituo cha Mjini FM, Belle 9 aliulizwa kuhusu sababu hasa zinazopelekea mashabiki kuwa na mawazo hasi pindi msanii mkubwa anapohusishwa kujiunga na WCB ambapo Belle 9 alidokeza kuwa mtazamo huo ni kutokana na watu kutokujua kwa undani kuhusu biashara ya muziki.
"Unajua record label kama Wasafi tuseme ukweli tu imefanya vizuri kuna wasanii inawezekana wangetumia muda mrefu kuwa pale kama wasingekuwa signed by mshkaji. Nadhani ni perception tu ya kibiashara watu hawana na hawataki kujifunza lakini pia vitu kama hivi watu wanapenda kuona vinatokea sehemu nyingine ndo watu watoe sifa. Wizkid kafanya hivi kafanya hivi. Hiyo" alidokeza Belle 9.
Ikumbukwe kuwa siku chache zilizopita Diamond Platnumz alidokeza kuwa kuna kipindi Marioo aliomba kujiunga na lebo yake ya WCB Wasafi, kitu ambacho siku chache baadae Marioo kupitia akaunti yake ya Instagram alikanusha na kusema kuwa Diamond alieleza kwa kusema vile.
Leave your comment