Harmonize Adokeza Ujio Wa Ngoma Mpya Na Abigail Chams

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Fundi wa muziki kutoka Tanzania ameanza mwaka 2023 kwa kasi ya aina yake baada ya kudokeza ujio wa ngoma mpya ambayo amemshirikisha Abigail Chams.

Kwa sasa nchini Tanzania, Harmonize anatamba na video mbili, Mwenyewe ambayo amefanya na Feza Kessy pamoja na Best Friend ambayo amemshirikisha Alice Kella na wakati watanzania wakiendelea kusafisha macho kupitia ngoma hizo, Harmonize hivi amedokeza ujio wa ngoma mpya kabisa na Abigail Chams kutokea Rockstar Africa.

Hivi karibuni CEO huyo wa Konde Music Worldwide kupitia uwanja wake wa Instastory, amedokeza kuhusu ujio wa collabo yake na Abigail  baada ya kuchapisha video akiwa anarekodi ngoma na Abigail Chams na kisha kuandika "Time Will Judge Abigail Chams" akimaanisha kuwa "muda ni utaamua"

Ikumbukwe kuwa Harmonize na Abigail Chams wameshashirikiana kwenye ngoma mbili tayari yaani Closer ambayo iliyotoka mwezi Agosti 2022 pamoja na Leave Me Alone, ngoma ambayo imepamba albamu ya tatu ya Harmonize ya kuitwa "Leave Me Alone"

Kufikia sasa bado Harmonize hajataja jina la ngoma hiyo, tarehe itakayotoka au taarifa yoyote ziada kuhusu mkwaju huo ambao unasubiriwa mno na mashabiki.

Leave your comment