Ubashiri Mechi ya Mlandege Vs Singida Big stars - Fainali Mapinduzi Cup- Mdundo Alt

[Picha:Singida Big stars Tz]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Klabu ya soka kutokea visiwani Zanzibar, Mlandege FC hatimaye baada ya zaidi ya Miaka 10 kwa timu kutokea Zanzibar imefanikiwa kutinga fainali za Kombe la Mapinduzi. Katika fainali hizo Mlandege watavaana na klabu ya Singida Big stars kutokea Tanzania bara siku ya Ijumaa.

Timu ya Mlandege ikiongozwa na mwalimu wake Mohammed Bares alisema ya kuwa usikivu pamoja na utulivu wa nafasi ndizo sababu zilizowafanya watinge fainali mara baada ya kumuondoa Namungo kwa mikwaju 5-4 ya penalti katika hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa timu ya Singida Big stars wao walifanikiwa kuingia fainali za kombe la Mapinduzi baada ya kumpa kichapo Cha bao 4-1 Azam huku mabao yote yakiwekwa kambani na Francy Kazadi.

Kocha msaidizi wa timu ya Singida Big Stars Mathius Lule amesema kuwa kwa sasa wanajiandaa katika fainali hizo Ili kuweza kuwadhibiti wapinzani wao.

Fainali hizi zimekuwa tunu kwa Mlandege haswa mara baada ya kuwa timu kutokea visiwani Zanzibar ambayo inashiriki fainali tangu mwaka 2012 huku bingwa mtetezi Simba akitolewa katika hatua ya makundi.

Kombe la Mapinduzi lilianzishwa mahususi kwa lengo la kusheherekea  Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea mnamo mwaka 1964 hivyo basi Odds za Singida Big stars kushinda mchezo huo ni 1.43.

 

 

 

Leave your comment