Nyimbo Mpya: Nikki Mbishi 'Price Up' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kama unapenda muziki mzuri kutoka Tanzania basi hii bila shaka hii itakuwa ni wiki nzuri sana kwako kwani wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania wameachia ngoma kali ambazo bila shaka zitakata kiu yako ya burudani.

Kutoka kwa wasanii kama Dizasta Vina, Nikki Mbishi na wengineo wengi zifuatazo ni ngoma kali kutoka Tanzania wiki hii :

Price Up - Nikki Mbishi

Nikki Mbishi ameendelea kuwakumbusha wapenzi wa muziki wa Hip Hop kuwa bado yupo vizuri kupitia "Price Up" ngoma ambayo ndani yake Nikki Mbishi anaonesha kuwa hadhi na thamani yake kama msanii imepanda huku akitoa mafunzo na darasa kuhusu maisha.

https://www.youtube.com/watch?v=TnhejSXXHf8

Homa 2 - Bando

Utapenda namna ambavyo Bando amecheza vizuri na maneno katika ngoma yake hii ya kuitwa Homa 2 ambayo kwa wiki hii imepeperusha vyema bendera ya muziki wa Hip Hop. Video ya ngoma hii pia imejaa ubunifu mkubwa na haichoshi kutazama.

https://www.youtube.com/watch?v=L99R-VXbIgU

Bless - B Gway

B Gway amerudi tena na ngoma yake hii ya kuitwa Bless. Kupitia ngoma hii B Gway anashukuru na kumpa utukufu Mwenyezi Mungu. Humu ndani B Gway pia ametajwa wasanii kama Harmonize, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba

https://www.youtube.com/watch?v=YNIqBowKJmI

Best Friend - Dizasta Vina

Wiki hii Dizasta Vina ameamua kuchangamsha game ya Hip Hop kwa kuachia Best Friend, ngoma ambayo wengi wameitafsiri kama jibu lake kwa Rapcha ambaye siku chache zilizopita aliandika diss track kumhusu Dizasta Vina.

https://www.youtube.com/watch?v=jUrvHEDyvT0

Fala Mimi - Frida Amani

Frida Amani anaonesha hasira, majuto na manyanyaso aliyopitia kupitia ngoma yake hii ya kuitwa Fala Mimi. Kwenye Fala Mimi, Frida Amani anamzungumzia mpenzi wake wa zamani na namna ambavyo alikuwa sio mwaminifu kwenye mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=E_em_qahLfc

Leave your comment