Diamond Platnumz Aweka Historia Youtube Kwa Mwaka 2022

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz kwa mara nyingine ameendelea kuonesha ukubwa wake kwenye muziki wa Tanzania baada ya kuweka rekodi ya aina yake kwa mwaka 2022 ndani ya mtandao wa Youtube.

Kwa mwaka 2022, Diamond Platnumz aliweza kupandisha ngoma mbalimbali kwenye akaunti yake ya  Youtube na aliweza kufikisha wafuasi au subscribers Millioni 7 katika akaunti yake ya Youtube na kuendelea kuwa msanii namba 1 chini ya jangwa la Sahara kuwa na idadi kubwa zaidi ya Subscribers.

Kwa mujibu wa Chart Data kwa mwaka 2022, ni kwamba Platnumz alikusanya jumla ya views au kutazamwa mara Milioni 448 na hivyo kuwa msanii kutoka Tanzania aliyetazamwa zaidi Youtube kwa mwaka 2022 huku video yake ya Mtasubiri ambayo imeshatazamwa mara Milioni 24 ikiwa ndio video iliyotazamwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2022.

Msanii wa pili kutazamwa zaidi Youtube ni Rayvanny ambaye alikusanya views Milioni 207 akifuatiwa na Harmonize ambaye alikusanya views Milioni 206 na kwa upande wa Zuchu akiwa amekusanya views Milioni 160.

Wasanii wengine pia waliotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mbosso, Marioo, Lavalava na Rose Muhando ambaye alisimama kuwa msanii wa Gospel kutoka Tanzania aliyetazamwa zaidi Youtube kwa mwaka 2022.

Leave your comment