TFF waingilia sakata la Feisal na Yanga

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Mara baada ya sakata lake la kutaka kuondoka Yanga, sasa Tanzania Football Federation (TFF) imeingikia kati suala hilo na kuandika barua kwa Feisal Salum Abdallah yenye lengo la kufanya mazungumzo na mchezaji huyo kuhusiana na sakata hilo.

Siku chache zilizopita kiungo huyo alibadilisha hali ya hewa mara baada ya taarifa za kutaka kuondoka Yanga kusambaa na Azam FC wakiwa wanahusishwa na taarifa za kutaka kumsaji mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili lililoanza Januari Mosi licha ya Azam kukana kuhusika.

Katika barua hiyo TFF wamemtaka Feisal kuwasili makao makuu ya shirikisho hilo la mpira wa miguu siku ya Jumatano ya tarehe 4 mwezi huu wa Januari yeye mwenyewe akifuatana na mwanasheria wake.

Young Africans Sport club wanaonekana kuwa na mamlaka juu ya kusalia kwa Feisal katika klabu hiyo mara baada ya mchezaji huyo kuthibitisha kubaki katika klabu hiyo siku chache baada ya taarifa za kuondoka klabuni hapo kusambaa.

Siku ya Jumanne mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram alisambaza picha zake zikimuonesha akiwa Dubai akiendelea na mazoezi tofauti na kikosi kizima Cha Yanga ambacho kwa sasa kiko Zanzibar.

Leave your comment