Diamond Platnumz,Rayvanny Wang'ara Kwenye Tuzo Za AEAUSA 2022

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mambo yameendelea kuwa sukari kwenye kiwanda cha Bongo Fleva na hii ni baada ya wasanii wakubwa Tanzania, Diamond Platnumz na Rayvanny kushinda tuzo za Africa Entertainment Awards USA hivi karibuni.

Tuzo za Africa Entertainment Awards USA maarufu kama AEUSA zilifanyika tarehe 31 Desemba mwaka 2022 kupitia njia ya mtandao ambapo wasanii tofauti tofauti waliweza kushinda tuzo hizo ambazo zina lengo la kuwatunuku heshima wasanii na wadau mbalimbali wa burudani Afrika.

CEO wa WCB, Diamond Platnumz aliweza kung'ara kwenye tuzo hizo baada ya EP yake ya First Of All maarufu kama FOA kuweza kushinda kipengele cha albamu bora ya mwaka Afrika na kushinda mbele ya Affection ya Magasco, Catch Me If You Can ya kwake Adekunle Gold, V ya kwake Asa kutokea Nigeria na nyinginezo nyingi.

Rayvanny pia alipeperusha bendera ya Tanzania kupitia ngoma yake ya Mama Tetema ambayo alifanya na Maluma ambapo alishinda kipengele cha Collabo bora ya mwaka kuoitia kipengele hicho. Katika kipengele hicho cha Collaboration, Rayvanny alikuwa anachuana na Peru ya Fireboy na Ed Sheran na nyinginezo.

Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni pamoja na Eddy Kenzo kutokea Uganda ambaye ameshinda kama msanii bora wa Afrika Mashariki huku Burnaboy kutoka Nigeria alishinda kama msanii bora wa mwaka.

 

 

Leave your comment