Diamond Platnumz Adokeza Ujio Wa  Video Ya 'Nitongoze'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya wimbo wa Nitongoze wa kwake Rayvanny akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz kufanya vizuri hatimaye Rayvanny anatarajia kuachia video ya ngoma hiyo hivi karibuni.

Ngoma ya Nidokeze iliachiwa mwishoni mwa mwaka 2022 ambapo ilikuwa ni ngoma ya kwanza ya Rayvanny tangu atangaze kuondoka WCB na tangu kuachiwa kwake Nitongoze imekuwa ni ngoma pendwa baina ya mashabiki ikiwa imeshasikilizwa mara Milioni 3.5 kwenye mtandao wa Youtube.

Hivi karibuni Diamond Platnumz amedokeza ujio wa Video Ya Nitongoze na hii ni baada ya msanii huyo kupost video kwenye Instastory yake akiwa location na Rayvanny ambapo aliisindikiza video hiyo na maneno yaliyosomeka "2023 won't be the same" hivyo kuashiria kwamba video hiyo huenda ikatolewa muda si mrefu.

Kando na Nitongoze, Rayvanny na Diamond Platnumz pia wameshashirikiana kwenye ngoma tofauti tofauti kama Salome, Mwanza, Tetema pamoja na Vumbi.

https://www.youtube.com/watch?v=e19CeM3H9ZM

Leave your comment