Nyimbo 10 Bora Ndani Ya mwaka 2022 Kutoka Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kitu kizuri kuhusu mwaka 2022 kwenye kiwanda cha muziki Tanzania ni kwamba, huu ni mwaka ambao ulikuwa hautabiriki. Wasanii wa kizazi kipya cha Bongo Fleva kama Jay Melody, Marioo, Platform na wengineo wengi wametoa "hits" za kutosha ambazo zimechangamsha muziki.

2022 ni mwaka ambao Zuchu na Diamond Platnumz waliwasubirisha mashabiki, Harmonize aliamua kubeba msalaba wake, Jay Melody alimtamkia mpenzi wake Nakupenda na Moyo wa Billnass ulidunda "Puuh" kutokana na mapenzi. Hakika tuliokota mengi sana mwaka huu.

Hizi hapa ni ngoma bora kutoka nchini Tanzania kwa mwaka huu wa 2022 :

Huyu Hapa - Mbosso

Mbosso kwa mara nyingine alithibitisha yeye ni mfalme wa ngoma za mapenzi kupitia Huyu Hapa. Huyu hapa ni ngoma ambayo imekuwa maarufu sana kwenye harusi na send offs nyingi sana Tanzania lakini pia kwenye mitandao kama Tiktok na Snapchat.

Kwa mwaka 2022 huu ndio wimbo mkubwa zaidi kutoka kwa Mbosso na pia wimbo huu unasimama kama moja ya ngoma bora za mapenzi kwa mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=uidtFhrkC8s

Napona - Nandy Ft Oxlade

Nandy alikuwa na mengi ya kufanya mwaka huu lakini hakutuacha wapweke mashabiki wa muziki kwani aliamua kumchukua Oxlade na kutupoza na Napona, ngoma ambayo ililenga kumpeleka Nandy kwenye soko la Nigeria.

Kiitikio cha "Napona" pamoja na mapokezano kati ya Oxlade na Nandy vimechagiza wimbo huu kuwa bora sana.

https://www.youtube.com/watch?v=73kHQmLaI9E

Champion - Kontawa Featuring Nay Wa Mitego

Kontawa alitetemesha nchi na ngoma ya Champion ambayo ndani yake alizungumzia maisha halisi ambayo watanzania wengi wanaishi. Wengi wamemfahamu Kontawa kupitia ngoma hii na kutokana na Champion kufanya vizuri sana, Harmonize pia aliamua kupamba remix ya ngoma hii.

https://www.youtube.com/watch?v=wgZwd2scJX0

Hadithi - Barnaba Featuring Diamond Platnumz

Kutoka kwenye albamu yake ya Love Sounds Different, Barnaba alitupatia Hadithi, wimbo ambao pia Zuchu alihusika katika kuuandika. Huu ni wimbo mzuri wa mapenzi ambao ulikata kiu ya mashabiki ambao walikuwa na hamu ya kumsikia Diamond Platnumz akiwa na Barnaba.

https://www.youtube.com/watch?v=-JaiCotheaU

Kwikwi - Zuchu

Salama Jabir mwaka huu alisema kwamba Zuchu ndio mwandishi bora wa kike wa muda wote na bila shaka wimbo huu ni ushahidi tosha wa kauli ile kwani Zuchu kupitia ngoma hii aliweza kuyasema ya sirini hadharani lakini kwa kutumia tafsida.

Kiitiko cha Kwikwi ni chepesi lakini kimeshonwa haswa na huu ni wimbo ambao umeimbwa na watu wa rika zote kuanzia watoto, wasichana, wavulana mpaka wanaume..

https://www.youtube.com/watch?v=Y2rdmKtVss0

Nitaubeba - Harmonize

Linapokuja suala la uandishi, Harmonize ni fundi na uhodari wake aliuonesha kwenye Nitaubeba, wimbo ambao Harmonize anatoa hadithi ya namna ambavyo mpenzi wake alimsaidia yeye kutoka kwenye nyakati ngumu za kimaisha.

Video ya Nitaubeba pia ilizua gumzo baada ya Kajala Masanja ambaye alikuwa mpenzi wa Harmonize kuwepo kwenye video hiyo

https://www.youtube.com/watch?v=ctZSzhBURiY

Mtasubiri - Diamond Platnumz ft Zuchu

Mtasubiri ni moja ya ngoma ambazo zilisubiriwa kwa hamu sana na kama ilivyokuwa kwenye Cheche na Litawachoma, wimbo huu pia ulionesha namna ambavyo wasanii hawa wawili wana vipaji vikubwa.

Kwa mwaka 2022 video ya Mtasubiri ndio video ya muziki  kutoka Tanzania iliyotazamwa zaidi Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=IokCG2J-_5Q

Puuh - Billnass Featuring Jay Melody

Kwa mara nyingine Billnass alithibitisha ukubwa wake kwa kuachia Puuh ngoma ambayo pamoja na kwamba ina miondoko ya Hip hop lakini mabinti wengi wameonekana kuipenda na kukubali hasa sehemu ya kiitikio.

Kwenye mtandao wa Youtube, Puuh ndani ya siku 12 tu tayari ilikuwa imeshafikisha watazamaji Milioni 1, jambo ambalo ni nadra sana kutokea kwa wasanii wa Hip Hop

https://www.youtube.com/watch?v=3qN9A3XIPcw

Naogopa - Marioo Featuring Harmonize

Marioo aliweza, kuwakosha haswaa mashabiki zake baada ya kuachia Naogopa ambayo amemshirikisha Harmonize. Marioo katika wimbo huu anavaa uhusika wa mwanaume ambaye hana kipato kikubwa na hivyo kumsihi mpenzi kuwa asimwache na kwenda kwa mwingine.

Ngoma hii ilipata umaarufu mkubwa pindi ilipoachiwa huku mashabiki wengi wakiwa wanashindwa Isha nani amefanya vizuri zaidi kati ya Harmonize na Marioo.

https://www.youtube.com/watch?v=LJONP5YAokU

Nakupenda - Jay Melody

Bila collabo wala kutegemea kiki Jay Melody mwaka huu aliwakosha wengi na "Nakupenda" wimbo ambao kufikia sasa umekuwa maarufu sana Tiktok na Snapchat. Kupitia Nakupenda Jay Melody amekuwa mkubwa zaidi na wimbo huu umetajwa kuwa ndio wimbo uliosikilizwa zaidi Tanzania kwa mwaka 2022 na majukwaa mbalimbali ya kusikilizia muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=LRdmZEdZ67g

Leave your comment

Top stories